Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
100.Surat Al-A'adiyaat

Imeshuka Makka Ina aya 11
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa


KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 01. Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua, 12. Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini, 23. Wakishambulia wakati wa asubuhi, 34. Huku wakitimua vumbi, 45. Na wakijitoma kati ya kundi, 56. Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! 67. Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo! 78. Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! 89. Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini? 910. Na yakakusanywa yaliomo vifuani? 1011. Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote! 11


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani