Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
101.Surat Al-Qaaria'h

Imeshuka Makka Ina aya 11
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa


KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 01. Inayo gonga! 12. Nini Inayo gonga? 23. Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga? 34. Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika; 45. Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa! 56. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, 67. Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. 78. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, 89. Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! 910. Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo? 1011. Ni Moto mkali! 11


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani