Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
102.Surat At-Takaathur

Imeshuka Makka Ina aya 8
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa


KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 01. Kumekushughulisheni kutafuta wingi, 12Mpaka mje makaburini!
3. Sivyo hivyo! Mtakuja jua! 34. Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua! 45. Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini, 56. Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu! 67. Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini. 78. Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema. 8


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani