Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
80.Surat A'basa

Imeshuka Makka Ina aya 42
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa


KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 01. Alikunja kipaji na akageuka, 12. Kwa sababu alimjia kipofu! 23. Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? 34. Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? 45. Ama ajionaye hana haja, 56. Wewe ndio unamshughulikia? 67. . Na si juu yako kama hakutakasika. 78. Ama anaye kujia kwa juhudi 89. Naye anaogopa, 910. Ndio wewe unampuuza? 1011. Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. 1112. . Basi anaye penda akumbuke. 1213. Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa, 1314. Zilizo inuliwa, zilizo takaswa. 1415. Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, 1516. Watukufu, wema. 1617. Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? 1718. Kwa kitu gani amemuumba? 1819. Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. 1920. Kisha akamsahilishia njia. 2021. Kisha akamfisha, akamtia kaburini. 2122. Kisha apendapo atamfufua. 2223. La! Hajamaliza aliyo muamuru. 2324. . Hebu mtu na atazame chakula chake. 2425. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu, 2526. Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu, 2627. Kisha tukaotesha humo nafaka, 2728. Na zabibu, na mimea ya majani, 2829. Na mizaituni, na mitende, 2930. Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara, 3031. Na matunda, na malisho ya wanyama; 3132. Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. 3233. Basi utakapo kuja ukelele, 3334. Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, 3435. Na mamaye na babaye, 3536. Na mkewe na wanawe 3637. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha 3738. Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri, 3839. Zitacheka, zitachangamka; 3940. Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi, 4041. Giza totoro litazifunika, 4142. Hao ndio makafiri watenda maovu 42


Sura Nyingine Faharasa

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani