Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
94.Surat Ash-Sharh'

Imeshuka Makka Ina aya 8
Utangulizi Sura Nyingine Faharasa


KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 01. 1. Hatukukunjulia kifua chako? 12. Na tukakuondolea mzigo wako, 23. Ulio vunja mgongo wako? 34. Na tukakunyanyulia utajo wako? 45. Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi, 56. Hakika pamoja na uzito upo wepesi. 67. Na ukipata faragha, fanya juhudi. 78. Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie. 8


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani