Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
95.Surat At-Tin

Imeshuka Makka Ina aya 8
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa


KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 01. Naapa kwa tini na zaituni! 12. Na kwa Mlima wa Sinai! 23. Na kwa mji huu wenye amani! 34. Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. 45. Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini! 56. Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha. 67. Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo? 78. Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote? 8


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani