Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
97.Surat Al-Qadr

Imeshuka Makka Ina aya 5
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa


KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 01. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. 12. Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri? 23. Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. 34. Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. 45. Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri. 5


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani