Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratush Sharh

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Hakika tumekukunjulia kifua chako kwa kuwa tulitia ndani yake Uwongofu na Imani.
Rudi kwenye sura

* 2. Na tumekupunguzia mizigo iliyo kuwa mizito juu ya mgongo wako, kwa kukuunga mkono na kukusahilishia mambo yako,
Rudi kwenye sura

* 3. Ambayo yalikuwa ni mazito juu ya mgongo wako.
Rudi kwenye sura

* 4. Na tumelitukuza jina lako, tukalifanya linatajwa na ulimi wa kila Muumini pamoja na jina letu.
Rudi kwenye sura

* 5. Hizo ni baadhi ya neema zetu juu yako. Basi kuwa na yakini na uweza wa Mwenyezi Mtukufu, kwani pamoja na uzito upo wepesi mwingi unao kuja nao.
Rudi kwenye sura

* 6. Hakika pamoja na uzito (wakati huo huo ijapo kuwa wewe hujui), upo wepesi mwingi vile vile.
Rudi kwenye sura

* 7. Basi ukipata nafasi katika kazi ya kuwalingania watu, na mambo yaliyo khusiana na Jihadi, endelea na jitihada ya ibada na jishughulishe nafsi yako katika hayo.
Rudi kwenye sura

* 8. Kwa Mola wako Mlezi tu ndio uelekee kwa kumwomba na kumhitajia.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani