Al Muddaththir Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
74.Surat Al-Muddaththir

Imeshuka Makka Ina aya 30
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1.Ewe uliye jigubika! 1


2.Simama uonye! 2


3.Na Mola wako Mlezi mtukuze! 3


4.Na nguo zako, zisafishe. 4


5.Na yaliyo machafu yahame! 5


6.Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa. 6


7.Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri! 7


8.Basi litapo pulizwa barugumu, 8


9.Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu. 9


10.Kwa makafiri haitakuwa nyepesi. 10


11.Niache peke yangu na niliye muumba; 11


12.Na nikamjaalia awe na mali mengi, 12


13. Na wana wanao onekana, 13


14.Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa. 14


15.Kisha anatumai nimzidishie! 15


16.Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu! 16


17.Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana. 17


18.Kwani hakika yeye alifikiri na akapima. 18


19.Basi ameangamia! Vipi alivyo pima! 19


20.Tena ameangamia! Vipi alivyo pima! 20


21.Kisha akatazama, 21


22.Kisha akakunja kipaji, na akanuna. 22


23.Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari. 23


24. Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa. 24


25.Haya si chochote ila kauli ya binaadamu. 25


26.Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar. 26


27.Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? 27


28.Haubakishi wala hausazi. 28


29.Unababua ngozi iwe nyeusi. 29


30.Juu yake wapo kumi na tisa. 30


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani