Ash Shams Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
15.Surat Ash-Shams

Imeshuka Makka Ina aya 15
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Naapa kwa jua na mwangaza wake! 1


2. Na kwa mwezi unapo lifuatia! 2


3. Na kwa mchana unapo lidhihirisha! 3


4. Na kwa usiku unapo lifunika! 4


5. Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga! 5


6. Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza! 6


7. Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza! 7


8. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake, 8


9. Hakika amefanikiwa aliye itakasa, 9


10. Na hakika amekhasiri aliye iviza. 10


11. Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao, 11


12. Alipo simama mwovu wao mkubwa, 12


13. Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. 13


14. Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. 14


15. Wala Yeye haogopi matokeo yake. 15


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani