Al Layl Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
92.Surat Al-Layl

Imeshuka Makka Ina aya 21
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Naapa kwa usiku unapo funika! 1


2. Na mchana unapo dhihiri! 2


3. Na kwa Aliye umba dume na jike! 3


4. Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali. 4


5. Ama mwenye kutoa na akamchamngu, 5


6. Na akaliwafiki lilio jema, 6


7. Tutamsahilishia yawe mepesi. 7


8. Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake, 8


9. Na akakanusha lilio jema, 9


10. Tutamsahilishia yawe mazito! 10


11. Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia? 11


12. Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu. 1


13. Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia. 13


14. Basi nakuonyeni na Moto unao waka! 14


15. Hatauingia ila mwovu kabisa! 15


16. Anaye kadhibisha na kupa mgongo. 16


17. Na mchamngu ataepushwa nao, 17


18. Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa. 18


19. Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa. 19


20. Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. 20


21. Naye atakuja ridhika! 21


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani