Al A'laq Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
96.Surat Al-A'laq

Imeshuka Makka Ina aya 19
Utangulizi Orodha ya Sura Faharasa

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0


1. Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, 1


2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, 2


3. Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! 3


4. Ambaye amefundisha kwa kalamu. 4


5. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui. 5


6. Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri 6


7. Akijiona katajirika. 7


8. Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo. 8


9. Umemwona yule anaye mkataza 9


10 . Mja anapo sali? 10


11. Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? 11


12. Au anaamrisha uchamngu? 12


13. Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? 13


14. Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? 14


15. Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! 15


16. Shungi la uwongo, lenye makosa! 16


17. Basi na awaite wenzake! 17


18. Nasi tutawaita Mazabania! 18


19. Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee! 19


Sura Nyingine Faharasa

Chagua Sura Nyingine:

Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani