Al Humazah maelezo
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Maelezo: Suuratul Humazah

Utangulizi:

Rudi kwenye sura

* 1. Atapata adhabu kali na maangamio huyo ambaye mtindo wake ni kuwafedhehi watu kwa kauli au kwa ishara, au kuwasengenya kuwavunjia hishima zao.
Rudi kwenye sura

* 2. Ambaye amekusanya chungu ya mali na akawa kazi yake kuyahisabu tu, kwa kuona ladha huko kuhisabu.
Rudi kwenye sura

* 3. Anadhani huyo kuwa mali yake yatamweka milele duniani, na yatamkinga na hayo anayo yachukia?
Rudi kwenye sura

* 4. Na aache dhana hiyo! Wallahi! Hapana shaka yoyote kwa vitendo vyake viovu hivyo atakuja tumbukizwa katika Moto unao vuruga kila kinacho tupwa humo!
Rudi kwenye sura

* 5. Na kitu gani kitacho kujuvya nini ukweli wa Moto huu wa H'ut'ama?
Rudi kwenye sura

* 6. Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa kwa amri yake, na daima unawaka!
Rudi kwenye sura

* 7. Ambao unafikilia nyoyoni na kuzizunguka nyoyo.
Rudi kwenye sura

* 8,9. Huo utakuwa umefungwa milango yake, na wao watakuwa wamefungwa humo ndani kwenye maguzo yaliyo nyooka. Hawawezi kutaharaki, wala kutoka.
Rudi kwenye sura

* 8,9. Huo utakuwa umefungwa milango yake, na wao watakuwa wamefungwa humo ndani kwenye maguzo yaliyo nyooka. Hawawezi kutaharaki, wala kutoka.
Rudi kwenye sura

Copyright © 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani